MBINU ANAZOTUMIA MAJOKA KUONGOZA SAGAMOYO NA MATAKWA YA WANASAGAMOYO KATIKA TAMTHILIA YA KIGOGO

Katika tamthilia ya Kigogo, Majoka kama kiongozo anatumia mbinu tofauti tofauti kuaongoza wana Sagamoyo.

Nao wana Sagamoyo wanayo matakwa wanayotaka kuotoka kwa viongozi wao.

Zifuatazo ndizo mbinu azitumiazo Majoka.

MBINU ANAZOTUMIA MAJOKA KUONGOZA SAGAMOYO

Kufuatia uchambuzi wetu wa tamthilia ya Kigogo, zifuatazo ndizo mbinu anazotumia Majoka ili kuaongoza Wanasagamoyo.

Uvumi.

Watu wa Majoka wanaeneza uvumi kuwa Sudi na Ashua ndio wanawinda roho ya Tunu.

Ahadi za uongo.

Madai ya Majoka kuwa atatoa chakula kwa wasiojiweza si ya kweli.

Kenga mshauri wa Majoka anawashawishi Sudi kuchonga kinyago cha Ngao ili apate malipo mazuri na maisha yake kubadilika.Kuwa jina lake litashamiri na apate tuzo nyingi zaidi ya hayo apate likizo ya mwezi mzima ughaibuni.Ahadi hizi zote ni za uongo.

Zawadi.

Kenga anawaletea Sudi, Boza na Kombe zawadi ya keki kuwafumba ili wamuunge mkono Majoka.

Vitisho.

Wanasagamoyo wanatishwa kwa kurushiwawa vijikaratasi wahame.

Majoka anatumia polisi kuwatisha wanasagamoyo.Matokeo yake ni watu kuhofia usalama wao.

Majoka anamtishia Chopi kuwa aramwaga unga wake kwa kutomamrisha polisi kutawanya waandamanaji.

Mapendeleo.

Ashua baada ya kufuzu kutoka chuo kikuu alipewa kazi katika Majoka and Majoka academy akakataa, sasa angekuwa mwalimu mkuu katika mojawapo ya shule za kifahari, viongozi hupendelea wengine kutumia njia sisizo halali.

Majoka alimpa Tunu kazi kiwandani akakataa.

Jela.

Viongozi hufungia wanaowapinga jela.Ashua anatiwa ndani,kuna washukiwa wengi ndani.

Polisi.Majoka anatumia polisi kutawanya waandamanahi wanaodai haki zao.

Viongozi hutumia nguvu.

Majoka anadai wafadhili wa wapinzani lazima wavunje kambi zao Sagamoyo, kuwa Sagamoyo yajiweza.

Anapanga kumkomesha Tunu dhidi ya kuongoza maandamano kutumia nguvu zake kiutawala.

Kenga anamshauri Majoka atangaze maandamano ni haramu kwa mutumia nguvu kisha maafisa wa polisi watumie nguvu zaidi.

Ulaghai.

Majoka anapanga kuongoza mishahara ya waalimu na wauguzi kwa aslimia kidogo kisha apandishe kodi.

Kudhibiti vyombo vya dora.

Majoka anapanga kufunga vituo vya runinga sagamoyo ili abakie na vichache anavyotaka vya kutangaza habari anazotaka.

Wavamizi.

Majoka anatumia wavamizi,Tunu anaumizwa mfupa wa muundi,Siti ana majeraha kutokana na uvamizi.

Ulinzi mkali.

Majoka nawatu wake wana ulinzi mkali. Kenga ana walinzi, Majoka analindwa na maafisa wa polisi.

Tunu na watu wake nanafurushwa wanapojaribu kukaribia soko la Chapakazi.

Kufuta kazi wasiomuunga.

Majoka anamfuta kazi kingi kwa kutomtii kupiga watu risasi sokoni Chapakazi.

MATAKWA YA WANASAGAMOYO.

  • Soko ambalo ni tegemeo lao linafungwa.Waataka soko lao lifunguliwe na kujengwa upya pia lisafishwe.
  • Hawana usalama,askari wanatumiwa kuwatawanya na kuwatishia.Wanaishi kwa hofu.
  • Hawana uhuru wa kutangamano kwani viongozi wao wahahofia maanamano.
  • Haki zao zimekiukwa.Mauaji yanapangwa kwa njama za kuwaangamiza.
  • Wanataka kujengewa hospitali, barabara na vyoo.Waletewe nguvu za umeme.
  • Wanataka wapate elimu Sagamoyo na ajira kwa vijana.
  • Wanasagamoyo wana njaa
  • Walimu na wauguzi Sagamoyo wana mishahara duni.
  • Kuna vilio Sagamoyo,mauaji yanapangwa.Wanasagamoyo wanataka mauaji haya yakome na haki kutendwa.
  • Wanasagamoyo wananyanyaswa na viongozi, bei ya chakula inapandishwa ilihali wengi wa wananchi ni maskini.
  • Mazingira Sagamoyo ni chafu hadi kuhatarisha maisha yao.Wanataka soko kusafishwa.

NEXT: MBINU ZA UANDISHI KATIKA TAMTHILIA YA KIGOGO


PREVIOUS:  MBINU MBINU ZA UANDISHI KATIKA TAMTHILIA YA KIGOGO


dhamira ya mwandishi katika kigogokigogo maudhuikigogo noteskigogo riwayakigogo setbook video downloadkigogo summarykigogo summary noteskigogo tamthiliakigogo tamthilia pdfkigogo videomaswali ya kigogomaswali ya tamthilia ya kigogomaudhui katika kigogo pdfmaudhui ya uzalendo katika kigogomwongozo wa kigogotamthilia ya kigogo videouchambuzi wa riwaya ya kigogowahusika wa tamthilia ya kigogo