MASWALI YA MAPAMBAZUKO YA MACHWEO NA HADITHI NYINGINE
-
FADHILA ZA PUNDA
- Kwa kutaja mifano mitano kutoka kwenye hadithi, Eleza ni kwa nini hadithi hii ikapewa anwani ya “Fadhila za punda”
-
Fafanua sifa za wahusika wafuatao kama zinavyojitokeza katika hadithi hii
- Luka
- Lilia
- Babake Lilia
- Luka
- Jadili nafasi ya mwanamke katika hadithi hii
- Eleza Dhamira ya mwandishi wa hadithi hii
- Taja na ueleze umuhimu za tamathali zozote Nne za lugha zilitotumika katika hadithi hii.
-
MSIBA WA KUJITAKIA
- Jadili maudhui yoyote matatu yanayojitokeza katika hadithi hii
- Jadili mbinu zozote nne za kimtindo zilizotumika katika hadithi hii
-
Eleza sifa na umuhimu wa wahusika wafuatayo
- Sugu Junior
- Machoka
- Zuhura
- Sugu Junior
- Eleza kikamilifu ni kwa nini jimbo la matopeni halijahuhudia maendeleo ya kisiasa tangu nchi kupata uhuru
-
MAPAMBAZUKO YA MCHWEO
- Jadili ufaafu wa anwani Mapambazuko ya Mchweo
- Eleza maudhui makuu ya hadithi hii
-
“….siyo Yule wa kujishaua mbele zako huku akifisidi rasilmali ya Nchi …..”
- Eleza muktadha wa dondoo
- Jadili jinsi wahusika mbalimbali wanazaofisidi rasilmali ya nchi katika hadithi hii
- Taja na ueleze tamathali ya usemi iliyotumika katika dondo hii
- Eleza muktadha wa dondoo
- Eleza changamoto za ukosefu wa ajira kama zinavyojitokeza katika hadithi hii
-
HARUBU YA MAISHA
-
Eleza kwa ufupi hadithi hii inahusu nini?
“Naja, nakamilisha shughuli ndogo hapa kisha nianze safari……”
- Weka dondoo hili katika muktadha wake
- Eleza sifa za msemaji wa kauli hii
- Weka dondoo hili katika muktadha wake
- Jadili changamoto wanazokumbana nazo waajiriwa kwa kurejelea hadithi hii
- Jadili umihimu wa matumizi ya dayalojia katika hadithi hii.
-
SABINA
- Eleza matatizo yanayomkumba mtoto wa kike kwa mujibu wa hadithi hii
- Je, unajifunza nini kutokana na hadithi hii
- Jadili mbinu tatu za lugha zilizotumiwa katika hadithi hii
-
MZIMU ZA KIPWERERE
- Eleza ni kwa nini mzimu wa kipwerere uliogopwa sana
- Jadili matumizi ya kinaya katika hadithi hii
-
Eleza sifa za wahusika wafuatao kama zinavyodhihirika katika hadithi hii
- Msimulizi
- Bishoo
- Salihina
- Msimulizi
- Je unajifunza nini kutokana na hadithi hii.
-
KILA MCHEZEA WEMBE
- Unafikiri ni kwa nini msimulizi amechagua kutumia barua kusimulia kisa chake
-
“ondoa wasi wasi mhibaka, you are in safe hands. Usiulize maswali its okey.tulikuja sote jana baada ya dance, umesahau hivi?”
- Fafanua muktadha wa dondoo hili
- Taja na ueleze mbinu za lugha zinazojitokeza katika dondoo
- Fafanua muktadha wa dondoo hili
- Jadili kwa kina madhara katika jamii kama yanavyodhihirika katika hadithi hii
-
Msiba ya kujitakia hauna kilio
- Eleza ukweli wa methali kama unavyojitokeza katika hadithi hii
- Taja na ueleze umuhimu wa tamathali nyingine nne za usemi zilizotumiwa katika hadithi hii
- Eleza ukweli wa methali kama unavyojitokeza katika hadithi hii
-
KIFO CHA SULUHU
- Eleza maana mbalimbali za kifo cha suluhu kama zinavyojitokeza katika hadithi hii
-
Fafanua maana na umuhimu wa tamathali zifuatazo za lugha kama zilivyotumika katika hadithi hii
- Methali
- Takriri
- Methali
- Jadili matumizi wa barua katika kuendeleza maudhui ya hadithi hii
- “kisasi hakifai” jadili hoja hii kwa kukita hoja zako kwenye matukio ya hadithi hii
-
AHADI NI DENI
- Jadili ufaafu wa anwani Ahadi ni deni katika hadithi hii
- Jadili umuhimu wa elimu kwa mototo wa kike kulingana na hadithi hii
- Eleza maana ya maudhui ya taasubi ya kiume yalivyoshughulikiwa katika hadithi hii
-
TOBA YA KALIA
- Unafikiri ni kwa nini hadi hii umepewa kichwa cha toba ya kalia?
- Jadili hasara ya ufisadi kwa kuzinngatia hadithi hii
- Eleza matumizi ya mbinu rejehi katika hadith hii
- Ukweli ndio mwanzo wa kupona kwa majeraha ya jadi! Jadili ukweli wa kauli hii kwa mujibu wa hadithi hii
-
NIPE NAFASI
- Eleza tafsiri tano ya kichwa cha hadithi hii ” Nipe Nafasi”
- Jadili matatizo yanayomkumba mwanamke katika jamii kwa mujibu wa hadithi hii
- Eleza ni kwa kiwango gani unakubaliana au kutokubaliana na mawazo ya wahusika wanaume kuhusu nafasi ya mwanamke katika hadithi hii.
- Unafikiri ni kwa nini mwandishi aliamua kutumia motto kusimulia hadithi hii
- Jadili mbinu zozote tano za kimtindo zilizotumiwa katika hadithi hii
-
NILITAMANI
- Taja vitu sita ambayo msimuliza anavitamani maishani
- ” tama mbele mauti nyuma” jadili ukweli wa kauli hii kwa kurejelea hadithi hii
- Unajifunza nini kutokana na hadithi hii
-
POPA
- Mwandishi wa hadithi hii anawatahadharisha watu dhidi kuwa na pupa maishani dhibitisha
- Umaskini umekuwa janga katika nchi nyingi zinazoendelea. Jadili kwa kurejelea hadithi hii
- Jadili maovu yanayoutendeka katika hadithi hii.
- Jadili matumizi ya mbinu ya majazi katika hadithi hii
-
Hadithi hii inahishia katika taharuki. fafanua