2019 KCSE KISWAHILI (102) KNEC REPORT

Hii ni ripoti ya utendaji wa KCSE ya Kiswahili ya 2019 kutoka Baraza la Mitihani la Kenya KNEC.
Ingawa matokeo ya jumla ya somo la Kiswahili katika mwaka wa 2019 yameimarika, utendaji wa asilimia kubwa ya wanafunzi unaelekea kuwa hafifu- Hili linadhihirika kwa matokeo ya karatasi ya tatu, ambayo yamekuwa yakishuka mwaka baada ya mwingine tangu 2016. Watahini wamekuwa wakishuhudia kushuka kwa viwango vya majibu yanayotolewa na watahiniwa. Kadhalika, kumekuwa na kushuka na kupanda kwa asilimia ya watahiniwa wanaotuzwa gredi za juu. Uchanganuzi huu unanuiwa kutathmini utendaji wa watahiniwa katika karatasi mahususi, na katika somo la Kiswahili kwa jumla. Jedwali lifuatalo linaonyesha matokeo ya mtihani wa somo la Kiswahili katika kipindi cha miaka minane (2012 hadi 2019).

Jedwali 9: Matokeo ya Mtihani wa Kiswahili (2012 – 2019)

Mwaka

Karatasi

Watahiniwa

Upeo

Alama ya Wastani

Alama

Tenganishi

2012

1

2

3

Jumla

433,886

40 80

80

200

10.43

29.06

32.14

71.62

3.63

10.77

15.15

25.71

2013

1

2

3

Jumla

445,555

40

80

80

200

18.46

29.92

34.82

83.19

5.44

12.68

14.92

29.77

2014

1

2

3

Jumla

482,122

40

80

80

20.17

32.27

42.93

9536

5.26

12.60

15.81

29.88

2015

1

2

3

Jumla

521,159

40

80

80

200

20.86

36.12

38.80

95.76

5.19

13.50

15.38

31.02

2016

1

2

3

Jumla

571,176

40

80

80

200

18.23

34.11

25.67

77-97

5.53

13-83

12.87

29.07

2017

1

2

3

Jumla

610,392

40

80

80

200

18.84 25.45

25.15

69.43

5.23

11.79

13.42

27.49

2018

1

2

3

Jumla

659,465

40

80

80

200

16.98

27.22

22_20

66.40

4.82

10.88

11.95

24.76

2019

1

2

3

Jumla

694,982

40 80 so

200

19.88

36.50

21.08

77.46

5.43

12.64

12.64

28.03

Kutokana na jedwali hili, pamoja na takwimu na ripoti nyingine za uchanganuzi wa karatasi za mitihani ya Kiswahili ya mwaka huu, imedhihirika kwamba kwa jumla:

  1. Utendaji wa wanafunzi katika utungaji umeimarika. Haya yanadhihirishwa na kupanda kwa alama wastani ya karatasi ya kwanza (102/1) kutoka 16.98 mwaka 2018 hadi 19.88 mwaka huu . Alama yajuu zaidi iliyotuzwa ni 37/40. Ni mwanafunzi mmoja tu ambaye alipata alama hii. Alama iliyotuzwa wanafunzi wengi (47,790) ni 23/40. Hali kadhalika, idadi ya wanafunzi ambao walipata asilimia sabini (70%) yaani 28/40 ilipanda kutoka 4,221 mwaka 2018 hadi 18,718 (2.69%) mwaka huu .
  2. Hata hivyo, changanuzi umedhihirisha kwamba bado kuna idadi ya wanafunzi (689) waliopata alama moja(1). Hakika wanafunzi 6,834 (0.98%) walipata baina ya alama I na 5. Pia karatasi ya kwanza bado haijawatenga vyema wanafunzi bora na wale hafifu. Hili linadhihirishwa na alama tenganisho (5.43. ) ambayo iko chini sana ikilinganishwa na alama ya tenganisho ya kikaida ( 15.00). Hali hii inaweza kusababishwa na watahini kuongozwa na kutawaliwa na mtazamo nafsi wakati wa kuzitathmini insha za watahiniwa na kuishia kuwaweka katika viwango sawa au vinavyokaribiana_
  3. Alama ya wastani yakaratasiya pili (102/2) imcpanda kwa pointi 9.28 kutoka 27.22 mwaka 2018 hadi 36.50 mwaka huu. Alama yajuu zaidi iliyotuzwa ni 76/80. Ni mwanafunzi mmoja tu ambaye alipata alama hii. Wanafunzi 180 walipata baina ya alama 70/80 na 76/80. Aidha alama iliyotuzwa wanafunzi wengi ( 20, 054) ni 38/80. Hali kadhalika, idadi ya wanafunzi waliopata asilimia sabini (70%) yaani 56/80 katika karatasi hii ilipanda kutoka 1,007 hadi 8,140 (1.17%). Aidha, imebainika kwamba karatasi hii iliweza kuwatenga vyema wanafunzi bora na wale hafifiLAlama tenganisho ilikuwa 12.64 kinyumena 10.88, ya mwaka 2018.
  4. Hata hivyo , bado kuna asilimia ya wanafunzi ambao walipata alama za chini- Kwa mfano, wanafunzi 3,616 walipata bainaya alama 1 na alama 5 . Hali kadhalika, ruwaza za matokeo zaonyesha kuwa matokeo ya karatasi hii yamekuwa yakiyumba tangu mwaka wa 2009. Alama ya wastani ilishuka kwa takriban alama kumi (IO) mwaka 2010, ikapanda kwa taknban kiwango hichohicho mwaka 2011 , na baadaye kushuka kwa alama kumi na nne nukta thelathini (14.30 ) mwaka 2012. Mwaka 2013 ilipanda kwa kiasi kidogo mno, mwaka 2014 lava 235, na mwaka 2015 kwa takriban alama 4. Mwaka 2016 alama ilishuka kwa takriban alama mbili. Mwaka 2017 alama hii ilishuka kwa zaidi ya alama 8. Mwaka 2018 alama wastani ilipanda kwa takriban alama 2 na mwaka huu imepanda kwa alama 9.28.
  5. Matokeo ya karatasi ya tatu (102/3) ya mwaka wa 2019 yameshuka kwa takriban alama 1.12 kutoka alama wastani 22.20 mwaka 2018 hadi 21.08 mwaka huu. Alama ya juu nidi iliytuzwa ni 72/80. Ni mwanafunzi mmoja tu aliyepata alama hii.. Alama iliyotuzwa wanafunzi wengi (25,895) ni alama 01/80 (3.73%). Hii inamaanisha kwamba wanafunzi hawa walipata sufuri katika kila swali. Aidha wanafunzi 79,732 (11.47%) walipata baina ya alama 1 na 5 jambo linalodokeza kwamba wanafunzi hawa hawakusoma vitabu vya fasihi. Hali kadhalika, ni wanafunzi 646 tu ambao walipata asilimia sabini ( 70%) yaani 56/80 katika karatasi hii. Hii ni asilimia ndogo mno ( 0.09%) ya watahiniwa 694,982 ambao walifanya mtihani huu.
  6. Alama wastani ya somo la Kiswahili kwa jumla imepanda kwa alama 11.06 kutoka 66.40 mwaka 2018 hadi 77.46 ya mwaka huu.
  7. Kadhalika asilimia ya watahiniwa wanaopata gredi A na A- ilipanda, japo haijafikia kiwango cha kuridhisha.
  8. Alama wastani ya somo hili bado haijafikia kiwango cha kuridhisha (100/200).

Uchanganuzi wa karatasi mahususi

Kiswahili  Insha (102/1)

Jedwali 10: Matokeo ya Karatasi ya kwanza ya miaka 2012— 2019

Mwaka

2012

2013

2014

2015

2016

2017

2018

2019

Alama ya Wastani

10.43

18.46

20.17

20.86

18.23

18.84

16.98

19.88

Alama ya Tenganisho

3.63

5.44

5.26

5.19

5.53

5.23

4.82

5.43

Jedwali hili laonyesha hvamba kwa kipindi cha miaka minne (2016 – 2019), ütendajİ wa watahiniwa katika karatasİ hü umekuwa ukiyumba. Tathminİ ya kazi halisi za watahiniwa İmebainisha kwamba asilimia kubwa ya watahiniwa haimudu kujielcza kwa lugha İliyokomaa. Ni wazi kwamba idadi kubwa ya watahiniwa haikuweza kukuza mada inavyostahili. Aidha, asilimia kubwa ya watahiniwa ililipata chini ya nusu ya alama zilizotengewa karatasi hİİ yaani 19/40. Tathmini ya kazi za watahiniwa pia imeonyesha kwamba watahiniwa wengi hawamudu tungo za kiuamİlİfu. Wengİ wanazingatia muundo wa tungo hizi bila kushughulıkia maudhuİ ya swali kikamilifu. Kwa nıfano ingawa swalİ la kwanza liliwahitaji watahİnİwa kuonyesha umuhİmu wa vyuo vya kiufundi, wengi walipotoka, walijadili mikakati ambayo serikali na washikadau wanapaswa kuzingatia ili kuviborcsha vyuo hivi. Kadhalika wanafunzi hawamudu maswali yanayoshughuIİkİa masuala mtambuko. Asilimia kubwa ya watahiniwa haikuweza kuonyesha umuhimu wao katika kujihakikishia usalama. Hii ni ishara kwamba wanafunzi wengi, ama wamekosa ubunifu, au hawana mazoca ya kusoma kwa kina na kwa mapana. Kadhalika imebainika kwamba swali linalohusu methali halipcndelewi na wanafunzi wengi. İdadi ya watahiniwa walioteua swali [ililohusiana na methali ilikuwa chini. Hili linadokcza kwamba ule mtazamo wa kijadi kuwa insha zinazohusu methali huwa ngumu bado umekİta mizizi.

Tazama uchanganuzi wa swali la kwanza ambalo ndilo lililokuwa la lazima.

            I.          Lazima

Wewe ni Mkuu wa Elimu katika kaunti ndogo ya Tuangaze. Andika hotiba utakayowatolca Maafisa wa Elimu na Walimu Wakuu kuhusu umuhİmu wa kustawisha vyuo vinanyotoa mafunzo ya kiufundi kazıka eneo lam

Swali hilİ lilimhitaji mtahiniwa kuandİka hotuba kuhusu umuhİmu wa vyuo vinavyotoa mafunzo ya kiufundi

Hata hivyo, tungoza watahiniwazilidhihirisha kwambawengİ wamekosa ubunİfu. Wengİ hawakuweza kujadiIİ hoja zilizotarajiwa; wakashindwa kukum mada kikamilifu. Ni muhimu kukumbuka kuwa watahiniwa walikosa ubunifu hata karika maswali yale mengine.

Imebainika kwamba wanafunzi wcngi hawasomi kwa mapana, hivyo hawadiriki kushughulikia masuala mtambuko İpasavyo katika tungo zao.

          Ushauri kwa walimu

Walimu wawatayarishe wanafimzi wao katika maeneo yote bila ubaguzi, kulingana na mahitaji ya silabasi ya Taasİsİ ya Ukuzaji Mitaala, Kenya (KICD).

Mapendekezo

  1. Walimu wazidi kuwapa wanafunzi mazoezi Zaidi katika uandishi wa kiuamilifu.
  2. Walimu watumie silabasi ya K.I.CD ili kuelekeza ufundishaji wao. Mwongozo unaotolewa na KNEC kuhusu mada na stadi zinazotahiniwa, pamoja na vitabu Vya Fasihi vinavyotahiniwa, utumiwe kujalizana na silabasi ya KICD.
  3. Wanafunzi wahimizwekusoma kwa mapana, na kwa kina (magazeti, majarida, kazi za kifasihi, na vitabu katika nyanja anuwai) ih kujifahamisha kuhusu matukio ya kila siku katika jamii na mazingira Yao, kitaifa na pia kima Hili litapalilia ubunifu wao na kuwawezesha kumudu maswali yanayohusu masuala mtambuko iwapo yatatahiniwa. Haitoshi kujifunga katika masuala yaliyo vitabuni pekcc.
  4. Wanafunzi waongozwe na kuelekczwa kuhusu mikakati ifaayo ya kufasiri maswali. kwa uangalifu mkubwa huku wakizingatia maneno muhimu.

Kiswahili  Lugha (102/2)

Jedwali 11: Matokeo ya Karatasiya pili (102/2) ya miaka 2012 hadi 2019

Mwaka

2012

2013

2014

2015

2016

2017

2018

2019

Alama Wastani

29.06

29.92

3227

36.12

34.11

25.45

27.22

36.50

Alama ya Tenganisho

10.77

12.68

12.60

13.50

13.83

13.42

10.88

12.64

Matokeo ya karatasi ya 102/2 yameimarika kutoka 27.22 mwaka 2018 hadi 36.50 mwaka huu. Swali la kwanza liliwatatiza baadhi ya watahiniwa; hawakumudu maswali yaliyowahitaji kutumia ujuzi wao kupata majibu. Haya ni maswali yanayolenga kukuza stadi za kiwango cha juu cha utambuzi kama Vile uchanganuzi, usanisi na tathmini. Tutachanganua swali la tatu.

  1. MATUMIZI YA LUGHA (Alama 40)

            (a)     Andika maneno yenye miundo ifuatayo: (alama 2)

(i)     irabu, konsonanti, konsonanti, irabu, konsonanti, irabu (ii) konsonanti, konsonanti, irabu, irabu

(b) Ainisha mofimu katika maneno yafuaatayo:  (alama 2)

(i)             asemavyo

(ii)           mwangwi

(c) Onyesha aina za nomino katika sentensi ifuatayo.  (alama 3)

Shule nzima ilifurahia ukarimu wa Shirika la Tugawane.

(d) Andika sentensi ifuatayo katika wingi.   (alama 1)

Seremala aliulainisha ubao huo ili kutengeneza kasha amuuzie mlinzi huyo.

(e)     Tunga sentensi ukitumia vivumishi vinavyotoa maana zifuatazo.

(i)         Nafasi katika orodha.  (alama l)

(ii)          Kutobagua. (alarna 1)

(f) Andika sentensi ifuatayo katika hah ya ukubwa. (alama 1)

Mtu huyo alifuata njia iliyomwelekeza mjini.

(g) Andika upya sentensi zifuatazo kulingana na maagizo bila kupoteza maana-

(i) Mhandisi alikarabati mtambO.

Mtambo ulikuwa kiwandani_

(Unganisha kuwa sentensi moja bila kutumia kiunganishi )                                                                              (alama 1)

(ii) Kembo alishona fulana hiyo vizuri sana (Tumia kielezi cha kiasi badala ya Vile vilivyopigiwa m5tari.)      (alama l)

(h) Andika sentensi ifuatayo katika usemi halisi. (alama 2)

Mkurugenzi alisema kwamba wangetoa nyongeza y-a mshahara mwaka ambao

(i) Geuza sentensi ifuatayo katika wakati uliopita hali timilifu. (alama I )

Ni wazi kwamba gharama ya maisha itapanda bei ya mafuta ikipanda.

(j) Andika sentensi ifuatayo hali yakinishi. (alama 1)

Badi huwa hapitii hapa, huenda usimpate.

(k)          Zuri ni kwa baya, aminifu ni kwa na vivu ni kwa(alama 2) (l)    Nomino zifuatazo zimo katika ngeli gani?    (alama 2)

(i) sukari…………………………………………………………

(ii) teo………………………………………………………

(m) Changanua sentensi ifuatayo kwa kielelezo cha mstari. (alama 2)

Mvua imepusa na watu wameanza kuondoka.

(n) Vyakula viliandaliwa- Vyakula vilikuwa na viinilishe muhimu.

 (Unganisha kuunda sentensi changamano.)          (alama 2)

(o) Bainisha yambwa na chagizo katika sentensi ifuatayo. (alarna 3)

Zumari alimtunzia Keto watoto hao kwa upendo.

(p) Tunga sentensi mbili kuOnyesha maturnizi mawili ya kiambishi ‘ku’ (alama 2)

(q) Ainisha vishazi katika sentensi ifuatayo. (alama 2) Usalama ukiimarishwa watalii wengi watakuwa wanazuru humu.

(r) Unaporidhika na jambo unasema hewala, unaposhangilia timu yako kwa kupata ushindi unasema………………………na unapotaka usikivu unasema (alama 2)

(s) Jepesi ni kwa rahisi, ukuta ni kwa _ „ na njia ni kwa — (alama 2)

(t) Tunga sentensi moja kutofautisha maana ya dua na tua.  (alama 2)

(u) Mzee Pumu ni mraibu wa vileo. Baada ya muda watoto wake wawili wanakuwa watumizi sugu wa vileo. Andika methali inayoweza kutumiwa kuelezea hali hii. (alama 1)

(v) Tunga sentensi ukitumia kiunganishi cha uteuzi. (alama l)

Maswali katika sehemu hii yalilenga mada mbalimbali za kisarufi kama zilivyopendekezwa kwenye silabasi.Maswali yalimhitaji mtahiniwa kutumia ujuzi wake wa dhana za kisarufi kujibu maswali aliyopewa. Imebaimka kwamba utendaji wa wanafunzi katika dhana za kimsingi za lugha kama Vile kuandika katika umoja, njeo, aina za maneno, na mnyambuliko wa vitenzi unaendelea kuwa hafifu. Kadhalika, watahiniwa wengi walipoteza alama katika masvcali maalum, hata ya ufahamu na ufupisho, kutokana na makosa ya sarufi na hijai. Wengine hawakumudu kuandika ufupisho ipasavyo; walinakili Yale yaliyokuwa katika kifungu, na kuishia kupoteza alama kwa kuzidisha idadi ya maneno. Isitoshe, wanafunzi wengi, japo walielewa sajili ya kidini hawakumudu kulishughulikia swali hili (swali la 4) kwa kina kwa kupungukiwa na hoja.

Mapendekezo

  1. Walimu waendelee kuwapa wanafunzi mazoezi katika vipengele vyote Vya kisarufi.
  2. Wanafunzi wasisitiziwe kwamba baadhi ya maswali ni ya stadi za juu kama Vile matumizi/ utekelezaji na usanisi. Wasitarajie kila mara kupata maswali ya kuchopoa majibu moja kwa moja kutoka kwenye vifungu au kukariri kutoka kumbukumbu zao.
  3. Wanafunzi wapewe mazoezi ya ufahamu na muhtasari mara kwa mara huku wakihimizwa kuzingatia mtirinko ufaao ili wapate kuzoea kutumia viunganishi kutiririsha hoja katika kujibu maswali ya muhtasari.
  4.  Walimu wasisitize vipengele v-ya kimsingi Vya sarufi kuanzia kidato cha kwanza hadi kidato cha nne.
  5. Mwelekeomsetokatikaufunmji uzingatiwe zaidi. Mathalan mwalimu anaweza kutumia Fasihi kufunzia mada tata za sarufi, kama Vile aina za sentensi. Hili litachangia katika kulihuisha somo la sarufi na kuwafanya wanafunzi kulichangamkia.
  6. Walimu na wanafunzi watalii maeneo yote ya sajili bila ya kujifunga kwa chache tu ambazo ni za kawaida.
  7. Masuala yote katika silabasi yafundishwe katika upana wayo bila kubagua.

KISWAHILI  FASIHI (102/3)

Jedwali 12: Matokeo ya Karatasiya tatu (102/3) ya miaka 2012 hadi 2018

Mwaka

Alamaya Wastani

2012

2013

2014

2015

2016

2017

2018

2019

32.14

34.82

42.93

38.80

25.67

25.15

22.20

21.08

AlamayaTenganisho

15.15

14.92

15.81

15.38

12.87

13.42

11.95

12.64

Matokeo haya yanaonyesha kuwa utendaji wa watahiniwa katika karatasi hii unaendelea kudorora. Idadi kubwa (25,895) ya wanafunzi ilipata alarna 1/80. Hali kadhalika, karatasi za watahiniwa zimebainisha kwamba changamoto kuu inayoukumba utendaji wa wanafunzi katika fasihi ni kutosoma vitabu viteule. Ithibati ya haya ni kuchanganya kwa wahusika; mtahiniwa akajadili sifa za mhusika mwingine badala za yule aliyelengwa na swali. Kadhalika karatasi zilibainisha kutomudu maswali ya kimuktadha, pamoja na Yale ambayo yanamhitaji mwanafunzi kujadili umuhimu wa vipengele Vya kiploti kama Vile mandhari na mbinu rejeshi katika kuvijenga vipengele vingine Vya kazi husika kama Vile wahusika na maudhui_ Yaelekea kwamba ujifunzaji wa fasihi simulizi ni hafifu. Watahmiwa wcngi hawakulimuidu swali la fasihi simulizi, hasa lile lilitowahitaji kuainisha wimbo na kujadili mbinu mwafaka kuzifanyia nyimbo za aina hii utafiti.

Hali kadhalika, tathmini ya karatæsi halisi za watahiniwa ilibainisha kwamba asilimia kubwa ya watahiniwa, hata Wale wanaopata alama za juu nidi katika karatasi hii, haimudu kuwasilisha hoja kwa njia komavu. Kazi za watahiniwa zimepwezwa na makosa mengi ya kisarufi, kimuundo na hijai. KadhaliE pameibuka mtindo wa kuwasilisha hoja kwa uf’upi mno, bila kuzilolea mifano kutoka matini huslka ya kifasihi. Hili linawafanya watahiniwa wengi kupoteza alama. Vile vile maswali ya ushairi yanaepukwa na watahiniwa wengi. Hata Wale wanaodiriki kuyafanya, wanaambulia alama za chmi. Imebainika kwamba baadhi ya masuala ya kirnsingi ya ushairi hayalUnzwi, hivyo yanapotokea katika mtihani watahiniwa wengi hupoteza alama. Wanafunzi wanaonekana kukariri dhana za kishairi bila kuzielewa. Hawamudu kutumia ujuzi wa dhana hizi kujibia maswali.

Tutachanganua swali la kwanza kwani ndilo lililokuwa la lazima.

A. Matei: Chozi la Heri

          1.        Lazima

(a) “Sasa haya ameyapa kisogo kufunguliwa kwa kituo hiki ni kama mana iliyomdondokea kinywani kutoka mbinguni_”

(i) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)

(ii) Bainisha tamathali mbili za usemi ambazo zimetumiwa katika dondoo hili. (alama 2)

(iii) Fafanua umuhimu wa mhusika anayerejelewa katika dondoo hili katika kuijenga riwaya hii. (alama 6)

(b) Jadili mikakati mwafaka ambayo vijana wanatumia kukabiliana na hali Yao ya maisha kwa kuwarejelea wahusika wafuatao_

(i) Chandachema (alama 4 )

(ii) Dick      (alama 4)

Hili lilikuwa swali la kimuktadha ambalo lilimhitaji mwanafunzi kuwa ameisoma riwaya na kuelewa Ploti ili kubainisha msimulizi na mandhari katika riwayaambamo kauli ilitolewa. Swali hili pia lihitaji mwanafunzi kuonyesha mwingiliano uliopo kati ya vipengele Vya kazi ya kifasihi, hasa umuhimu wa wahusika katika kuijenga kazi ya kifæslhi.

Hata hivyo uchanganuzi wa utcndaji wa wanafunzi katika swali hili, na hata katika maswali mengine ulidhihirisha kwamba wanafunzi hawasomi vitabu Vya fasihi kwa kina. Watahiniwa hawakuweza kuliweka dondoo katika muktadha. Pia, hawakuweza kufafanua umuhimu wa wahusika. Kadhalika, wanafunzi wengi hawazielewi istilahi za kimsingi za uchambuzi wa kazi za kifasihi. Kwa mfano, watahiniwa wengi walishindwa kuelewa maana ya mtindo katika swali lilowahitaji kuchanganua vipengele kimtindo katika dondoo walilopewa.

MAPENDEKEZO

i) Walimu wawaongoze wanafunzi kujifunza vitabu vilivyoteuliwa kwa ukamilifu huku wakizingatia vipengele Vya uchanganuzi wa kazi za kifasihi:

a) Dhamira na maudhui

b) Fani, kama vile:

    • Mandhari- Maana na umuhimu wayo
    • Ploti- vipengele kama Vile mbinu rejeshi, elekezi na sadfa, na umuhimu wavyo
    • Usimulizi- nafsi na wakati katika usunulizi
    • Wahusika- Sifa na urnuhimu wao katika kuzijenga kazi za kifasihi
    • Muundo- urudiaji, usambamba._..
    • MtindO, kama Vile tamathali za usemi, urudiaji,

ii) Wanafunzi wahimizwe kutambua masuala muhimu yanayojitokeza katika hadithi zote katika diwani teule hadithi fupi.

iii) Wanafunzi wawekewe misingi Bora katika Fasihi Simulizi tangu kidato cha kwanza na kuongozwa kujiimarisha katika mada zote za fasihi simulizi kulinganana upeo uliopendekezwa na, mtaala wa Shule za upili.

iv) Walimu wawaelekeze wanafunzi wao kutambua na kutumia istilahi muhimu ushairi ili kuupalilia ukakamavu wao katika kuyajibu maswali ya Ushairi.

v) Mbinu za kuchanganua Ushairi zifunzwe katika upana na kina kulingana na kiwango hiki.

vi) La muhimu Zaidi wakumbushwe kwamba vipengele Vya kazi ya kifasihi havitofautiani. Mathalani, taswira na toni huweza kuchanganuliwa katika Ushairi, na vilevile katika tamthilia na tungo za kinathari, kama Vile riwaya

Hitimisho

Kutokana na uchanganuzi wa hapojuu, ni dhahiri kwambajapo utendaji wa wanafunzi katika somo la Kiswahili kwajumla umeimarika mwaka huu, matokeo ya karatasi ya tatu bado yanaendelea kushuka. Asilimia kubwa mno ya watahiniwa imepata tuzo za chini, hali ambayo imeshusha alama ya wastani ya karatasi hii na ya Somo Zima- Vilevile ni dhahiri k•wamba matokeo ya watahiniwa katika Somo la Kiswahili kwajumla bado hayajafikia kiwango cha kuridhisha.

Inatumainiwa kwamba walimu na wanafunzi watafaidi kwa uchanganuzi uliotolewa. Kadhalika ni muhimu kuyatilia maanani mapendekezo yaliyotolewa katika ripoti hii ili kuimarisha matokeo ya somo hili. Muhimu Zaidi, ipo haja ya kuandaa warsha na makongamano ili kufanikisha kujadiliwa kwa mada na stadi ambazo zinaelekea kuwatatiza Zaidi walimu na wanafunzi.


READ MORE KNEC REPORTS


Download free Education Materials Below


 

2019 KCSE Kiswahili Report2019 KCSE ReportsKCSE History PerformanceKCSE KNEC ReportsKiswahiliKiswahili ReportKNEC Kiswahili 2019KNEC Report
Comments (1)
Add Comment