Teacher.co.ke
Latest Education News, Free School Notes, and Revision Materials

WAHUSIKA KATIKA TAMTHILIA YA KIGOGO

Kunao wahusika kadhaa katika tamthilia ya Kigogo. Hawa ndio wahusika, na sifa kuwahusu.

MAJOKA

Ni kiongozi wa jimbo la Sagamoyo.

Ni katili.

Anaamuru Tunu auliwe,anavunjwa mfupa wa muundi.

Anamwambia kingi awapige watu risasi katika soko la Chapakazi.

Ni mkware.

Anapanga njama ya kumpata Ashua, anamtaka kimapenzi licha ya kuwa na mke na mtoto.

Ashua anapofika ofisini mwake,anataka kumkumbatia na kumbusu.

Mwenye hasira.

Anakasirika Ashua anapokataa asimkumbatie na kusema kuwa hasira yake imeanza kufunganya virago.(uk 20)

Mwenye majisifu.

Majoka anataka sifa, anauirahi sana Ashua anapomwita Ngao jina lake la ujana.

Anajisifu kuwa yeye pia anajua kuzaa na wala si kuzaa tu bali kuzaa na kulea.(uk22)

Mwenye dharau.

Anawadharau watoto wa Ashua kwa kuwaita vichekechea.(uk22)

Anamdharau Sudi mumewe Ashua kwa kumwita zebe.

Anamdharau Tunu kuwa ni daktari na hana kazi ya maana.

Tunu anapokataa poza ya Ngao Junior anamdharau kuwa msichana mdogo hata ubwabwa wa shingo haujamtoka.

Mpenda anasa.

Majoka anamwambia Ashua asilie bali aseme na ampendaye,astarehe kwenye kifua cha shujaa wake.(uk22)

Anataka kumpa Ashua huba,anamwita muhibu wake.(uk21)

Mnafiki.

Anamwambia Ashua kuwa,

“…haja zako ni haja zangu, shida zako ni shida zangu na kiu yako ni kiu yangu.”

Nia yake ni kumteka Ashua kimapenzi, hana moyo wa kujali.

Anadai kuwa hapendi rafu Ashua wanapopigana na Husda ofisini huku ni yeye huzua rafu Sagamoyo kwa kupanga mauaji hadi watu kuandamana.

Mpyoro.

Anawatusi wanasagamoyo kuwa wajinga katika soko la Chapakazi.

Anamwita Sudi mumewe Ashua Zebe.

“…uliona nini kwa huyo zebe wako.” (uk24)

Mwenye kiburi.

Anajiita mwana wa shujaa kwamba ana akili ndipo kuwa mwana wa shujaa.Anasema kuwa aliitwa Ngao kwa kuwa na sifa.

Anajifananisha ma Samsoni Myaudi na shujaa Lyona wa Waswahili.

Anadai kuwa Ashua amembandika jina la kumkwaza kwa kumwita mzee.

Ni katili.

Anamfungia Ashua licha ya kumwomba msamaha kuwa ananyonyesha.

Anapanga njama za mauaji bila kujali haki za raia.

Anawafungia wanasagamoyo soko ambalo ni tegemeo lao biala kujali.

Ni dikteta.

Majoka hutoa amri,polisi watawanye waandamanaji.

Kenga anasubiri amri ya Majoka ili amkomeshe Tunu kufanya uchunguzi kuhusu kifo cha Jabali.

UMUHIMU WA MAJOKA

Ametumika kuonyesha jinsi ambavyo viongozi hutumia mamlaka yao vibaya kunyakua ardhi ya umma,kuvunja sheria za katiba,kudhibithi vyombo vya dora, kupanga njama za mauaji,kunyanyasa maskini na kudhulumu wnawake kimapenzi.

Ni kielelezo cha viongozi katika mataifa yanayoendelea na shida zinazoyakumba kutokana na uongozi mbaya.

TUNU

Ni mwanamke Sagamoyo ambaye anapinga maovu ya Majoka,rafikiye Sudi na mtoto wa Hashima.

Ni mwanamapinduzi.

Anaongoza maandamano Sagamoyo.

Anahutubia wanahabari kuhusu hali halisi Sagamoyo.

Anakiri kutolegeza msimamo wao hadi soko lifunguliwe.

Ni msomi.

Ana shahada ya sheria kutoka chuo kikuu.

Ni mtetezi wa haki .

Anapanga kuleta wachunguzi kutoka nje ili kuchunguza kuhusu kifo cha Jabali .

Anamwambia Majoka wazi kuwa kila mtu Sagamoyo ana haki nya kuishi.

Mwenye msimamo dhabiti.

Anakataa wazo la Majoka kumwoza kwa Ngao Junior.

Licha ya kuumizwa mguu, halegezi kamba kuwapigania wanasagamoyo.

Ni jasiri.

Haogopi yeyote, anataka kukutana na viongozi katili ili awakashifu.

Anamwambia Majoka wazi kuwa hawezi kuolewa na mhuni,kwanba wanakula watu kwa jina la ugatuzi.(uk42)

Ni mzalendo.

Tunu anapigania haki za Wanasagamoyo, anamwambia Majoka kuwa wanasagamoyo wana haki ya kuishi na kuwa ugatuzi si unyakuzi.

Mdadisi.

Anamdadisi mamake ili ajue maana ya ndoto ya Mzee Marara kumfukuza ili amnyanganye mkufu wake wa dhahabu.

Anapanga kuchunguza ajali iliyosababisha kifo cha Tunu.

Mwajibikaji.

Tunu amawajibika, anaelewa athari ya pombe,na kukataa pombe anayopewa kwa mamapima.

Mwenye usawa

Anapigania usalama wa kila mtu Sagamoyo,habagui yeyote.Hambagui mamapima anapomwomba msamaha.

UMUHIMU WA TUNU.

Tunu ametumika kuonyesha kuwa kuna wazalendo katika jamii ambao wamejitolea kupinga uongozi mbaya ili kuleta haki na usawa katika jamii.

Mwandishi amemtumia mhusika Tunu kuonyesha kuwa licha ya changamoto zinazomkumba mtoto wa kike, bado ana nafasi muhimu katika ujenzi wa jamii mpya, wanawake ni muhimu katika uongozi ili kuleta maendeleo.

ASHUA

Ni mkewe Sudi,mamake Pendo na Pili

Ni mwenye msimamo thabiti.

Licha ya kushawishiwa kimapenzi na Majoka, hakubaliani na kauli yake.Anashikilia msimamo wake kuwa ana mume na hataki kuvunja ndoa yake,anakataa huba kutoka kwa Majoka.

Ni jasiri.

Anamkabili Majoka kwa kupasa sauti ofisini mwake,haogopi.Anamwambia kwa ujasiri kuwa anefika kwake kuomba msaada.

Ni mnyenyekevu.

Ananyenyekea mbele ya Majoka ofisini mwake na kumwomba msamaha,anamwomba Majoka amkanye Husda asimtusi.

Ni mwenye heshima.

Anakiri kuwa anamheshimu Majoka.

Ni mwaminifu.

Ashua ni mwaminifu katika ndoa yake. Anakataa kufanya mapenzi na Majoka kwa kuhofia talaka yake.

Anathamini ndoia yake, anakataa pendekezo la Majoka kwa madai kuwa yeye ni mke wa mtu.

Ni msomi.

Ashua amesoma na ana shahada ya ualimu.

Amezinduka.

Anadai kuwa kampuni ya Majoka ni ya wahuni.Anaelewa kuwa wanasagamoyo wamenyanyaswa hivyo kujiunga na wanamapinduzi kupigania haki.

Ni mkali.

Ashua anamkabili Husda kwa ukali ofisini mwa Majoka.

Ni mwenye tamaa.

Ashua baada ya kutiwa ndani kwa Majoka,tamaa inamjaa.Anamwambia Sudi kuwa amechoka kupendwa kimaskini,tamaa ya mali inamtawala.

Asiye na subira.

Subira inamhama Ashua.Hawezi kusubiri hadi Sudi awe na uwezo wa kumtunza.

UMUHIMU WA ASHUA.

Ametumika kuwakilisha wanawake ambao wanathamini na kuzienzi ndoa zao, wanawake waaminifu lakini kwa sabavu ya kutawaliwa na tamaa ya mali na ubinafsi,huaribu ndoa zao.

SUDI.

Ni mumewe Ashua, fundi wa kuchonga vinyago Sagamoyo ambaye anashirikiana na Tunu kupinga maovu ya Majoka.

Ni mzalendo.

Kwake taarifa za Majoka hazimfai, za kutangaza mashujaa waliopigania uhuru Sagamoyo.

Haoni maana ya uhuru huo hivyo kutomuunga mkono.

Ana jukumu la kulinda uhai, kulinda haki na kulinda uhuru.

Wanaitaji kuandika historia ya Sagamoyo upya.

Ni mwenye bidii.

Anafanya kazi ya kuchonga vinyago kwa bidii.

Ni mwenye msimamo thabiti.

Licha ya kushawishiwa na kuhaidiwa mengi na Kenga ili achonge kinyago cha Ngao, anakataa na kushikilia msimamo wake.

Ni jasiri.

Anamwambia Kenga kwa ujasiri wamemulikwa mbali.(uk12).

Haogopi kuchonga kinyago cha mwanamke.

Amezinduka.

Hali keki ya uhuru wanayoletewa na Kenga kwa madai kuwa ni makombo.Anaelewa kuwa viongozi wanawanyanyasa.

Ni mwajibikaji.

Sudi amewajibika,anajitahidi kwa udi na uvumba ili kumkidhi Ashua. Kila kitu anachokipata humletea Ashua.

Ni mwenye mapenzi ya dhati .

Sudi anampenda mkewe kwa dhati. Hufanya kila kitu ili kumkidhi.

Ni mwaminifu.

Sudi ni mwaminifu katika ndoa yake.Anampenda Ashua na anajelea kumpa talaka Ashua anapoiomba.

Ni msomi.

Sudi ana shahada, walisoma shule moja na Tunu.

UMUHIMU WA SUDI.

Mwandishi amemtumia mhusika Sudi kuonyesha kuwa kuna,wazalendo katika jamii ambao wamejitolea kuoigania haki ili kujenga janii mpya, watu ambao wamejitolea kupinga uongozi mbaya.

KENGA.

Ni mshauri mkuu wa Majoka.

Ni mshauri mbaya.

Anamshauri Majoka visivyo.Anamwambia atangaze kuwa maandamano ni haramu kisha aamuru maafisa wa polisi watumie nguvu zaidi.

Ni kikaragosi.

Anamuunga Majoka mkono hata kwa mambo yasiyofaa nia yake ikiwa ni kujinufaisha kutokana na uongozi wake.

Ni fisadi.

Yeye na Majoka wanadai kitu kidogo kutoka kwa wanasagamoyo.

Baada ya soko kufungwa,Majoka anamwambia kuwa kipande chake cha ardhi kipo.Anakipata kwa njia isiyo halali.

Ni mwoga.

Kenga abahofia maandamano yanayoendelea na kumshauri Majoka asiyapuuze

Ni mwenye matumaini.

Hafi moyo, anasema atarudi tena na tena ili kusema na Sudi ili achonge kinyago.

UMUHIMU WA KENGA.

Kenga anawakilisha washauri wabaya wa viongozi katika jamii, watu ambao nia yao ni kujinufaisha wenyewe bila kujali maslahi ya wanyonge.

Washauri ambao ni katili na hata hupanga njama za mauaji ili kuendelea jufaidi kutoka kwa viongozi.

NGURUMO.

Ni kijana mpenda anasa, mfuasi wa Majoka.

Ni mlevi.

Ngurumo ni mlevi kupindukia,anajulikana Sagamoyo kutokana na ulevi wake.

Ni msaliti.

Anasaliti wanamapinduzi kwa madai kuwa Sagamoyo ni pazuri tangu soko kufungwa.

Anasaliti katiba ya nchi yake kwa kunywa pombe haramu, kinyume na sheria.

Ni mpenda anasa.

Ngurumo anapenda anasa, kwake kulewa ni starehe.

Mwenye taasubi ya kiume.

Anamdharau Tunu kwa kuwa mwanamke,anadai kuwa yeye si kitu Sagamoyo.

Anamwimbia wimbo wenye ujumbe kuwa aolewe ili asije akazeekea kwao

Ni kikaragosi.

Yeye ni mfuasi wa Majoka,anaunga uongozi wake mkono licha ya kuwa haufai.

UMUHIMI WA NGURUMO.

Mwandishi amemtumia Ngurumo kuonyesha kuwa kuna vijana ambao wamepotoshwa na anasa katika jamii na kukosa mwelekeo.Ngurumo ni kijana lakini mlevi kupindukia.

BOZA

Ni fundi wa kuchonga vinyago Sagamoyo, mumewe Asiya(mamapima)

Ni mwenye hasira.

Anamwambia Sudi kwa hasira kuwa embe lake linanuka fee.(uk1)

Ni kikaragosi.

Anatetea viongozi kuwa ni jukumu lao kusanya kodi, kuwa huku ndilo kujenga nchi na kujitegemea.(uk3)

Anafurahia wimbo wa uzalendo unaosifia uongozi wa Majoka ilhali hali ni tofauti Sagamoyo kulingana na maudhui katika wimbo huo.

Anamuunga Majoka mkono ili afaidi.

Mwenye majisifu.

Anajisifu kuwa keki ya uhuru imeokwa na mke wake mwenyewe.

Ni msaliti.

Anawasaliti wanamapinduzi kwa kuunga mkono uongozi Mbaya wa Majoka mkono.

UMUHIMU WA BOZA.

Boza ametumika kuonyesha watu ambao hawajazinduka katika jamii,wanaotumikizwa na viongozi na kufumbwa kwa mambo madogomadogo ili waendelee kuunga uongozi mbaya mkono.

HUSDA

Ni mkewe Majoka.

Ni mwenye tamaa ya mali.

Anaolewa na Majoka kwa sababu ya pesa na wala si mapenzi halisi

Ni mkali.

Anasema atamuua mtu anapompata Ashua na Majoka.

Mpyoro.

Anamtusi Ashua na kumwita kidudumtu na mdaku.

Mbinafsi.

Husda ana ubinafsi,anaolewa sababu ya mali ili kujinufaisha.

UMUHIMU WA HUSDA.

Husda ni kielelezo cha wanawake wanaoongozwa na tamaa ya mali hata hata katika ndoa,wanawake wanaoolewa kwa sababu ya mali na wala si mapenzi ya kweli.

MAMAPIMA

Huyu ni Asiya mkewe poza anayeuza pombe Sagamoyo.

Ni laghai.

Anawapunja walevi.

Ni mwenye tamaa ya pesa.

Anawapunja walevi kwa sababu ya tamaa ya pesa.

Amekiuka sheria.

Anauza pombe haramu kinyume cha sheria.

UMUHIMU WA MAMAPIMA.

Mamapima ametumika kuonyesha watu ambao huongozwa na tamaa hadi kiwango cha kukiuka sheria.

BABU.

Ni babuye Majoka ambaye ametokea ndotoni.

Ni mshauri mwema.

Anamshauri Majoka abadili mienendo yake na asikie vilio vya wanasagamoyo na aone maovu aliyoyatenda.(uk 83)

Ni mwenye hekima.

Anathibitisha kauli kuwa maisha ni mabadiliko na maovu yana mwisho.

Anamwonya Majoka dhidi ya kuishi kwa kutojali, kuwa hasara itamwandama akataliwe na watu asiwe mtu tena.

Anampa Majoka wosia kuwa binadami ni mavumbi na atarejea mavumbini kwa hivyo asihishi kwa kuwanyanyasa wengine wala asiongozwe na tamaa maishani.

Anamshauri kuwa mkwea ngazi huteremka.(uk84).

Anamwambia Majoka atende wema daima na ataishi maisha mema iwapo atakufa, atajiandikia tarijama njema huko ahera.

UMUHIMU WA BABU.

Mwandishi wa tamthilia ya Kigogo amemtumia Babu kuonya umma kuwa si vyema kutendea wengine mabaya, maana maovu yana mwisho.Wanadamu wasiishi kwa kuwanyanyasa wengine wala kuongozwa na tamaa bali watende mema daima.


NEXT: MAUDHUI KATIKA TAMTHILIA YA KIGOGO


PREVIOUS: MTIRIRIKO KATIKA TAMTHILIA YA KIGOGO


Comments are closed.

CHECK DOMAIN